Mwanamke anataka kusafiri na washemeji na mama mkwe


Swali: Mimi naishi na familia ya mume wangu. Watasafiri safari ndefu. Siwezi kubaki mwenyewe na mume wangu hayupo. Je, nisafiri nao ikiwa ni ndugu na mama wa mume wangu? Mume wangu amekubali lakini hata hivyo hawezi kuwepo kwa sababu anafanya kazi mbali. Siwezi kusafiri naye na wala siwezi kubaki mwenyewe kwenye nyumba ya familia ya mume wangu.

Jibu: Ndugu wa mume wake sio Mahaarim zako. Usisafiri na yeyote isipokuwa Mahram wako. Ima mume wako aje na usafiri naye au baki kwenye mji mpaka pale atapokuja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018