Mwanamke ametwaharika ndani ya ndege


Swali: Mwanamke ametwaharika na hedhi yake wakati yuko msafiri kwenye ndege. Anataka kuswali. Je, inatosha kwake kutawadha?

Jibu: Hapana. Asubiri mpaka pale atapodema kutoka ndani ya ndege. Baada ya hapo aoge na kuswali. Na ikiwa safari ni ndefu na anachelea wakati wa swalah kutoka, afanye Tayammum kwa vumbi atayopata na aswali. Na ikiwa hakuna vumbi aswali vile atavyoweza hata kama hatojitwaharisha:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt--15041434.mp3
  • Imechapishwa: 19/03/2017