Mwanamke aliyeomba talaka hana haki ya mirathi ya mume


Swali: Je, Talaka inapita ikiwa mke atamuomba Talaka mume wake naye yuko katika hali ya ugonjwa?

Jibu: Ikiwa mke ndio kamuomba Talaka mume, Talaka inapita kwa hali yoyote. Lakini je, mke atarithi au harithi? Ikiwa mke ndio kamuomba, Talaka inapita lakini hatorithi. Na kama si yeye aliyemuomba, inapita na atarithi. Mu´amala kutokana na makusudio yake. Hata hivyo, Talaka inapita kwa hali yoyote. Lakini ikiwa yeye ndio kaiomba, inapita na wala hana haki ya mirathi kwa kuwa hastahiki mali yake. Ama ikiwa si yeye ndio kaiomba, Talaka inapita lakini hii halitomzuia kupata mirathi.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10069
  • Imechapishwa: 24/02/2018