Mwanamke aliyekuwa na hedhi kuamka na swawm

Swali: Kuna mwanamke ametwaharika na hedhi kabla ya adhaana ya Fajr na hakuoga isipokuwa baada ya adhaana. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Ndio. Swawm haishurutishi kuoga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaamka hali ya kuwa ana janaba na anafunga, kisha anaoga baada ya Fajr baada ya kuwa na swawm. Swawm haishurutishi twahara. Inajuzu kwa mtu kunuia swawm bila ya kuwa na twahara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14085
  • Imechapishwa: 16/11/2014