Mwanachuoni wa ki-Ibaadhiy akimkufurisha ´Abdullaah bin Sallaam

Swuhayb  amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watapoingia watu wa Peponi Peponi basi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atasema: “Je, kuna kitu mnataka nikuzidishieni?” Watasema: “Je, hukuzifanya weupe nyuso zetu? Hukutuingiza Peponi na Ukatuokoa kutokamana na Moto? Kisha Atafunua pazia Yake. Hawajapatapo kupewa kitu kama kumtazama Mola wao (´Azza  wa Jall).”[1]

Hadiyth hii na mfano wake si hoja kabisa kutokana na sababu nyingi kukiwemo:

Sababu ya kwanza: Mapokezi yote haya cheni za wapokezi wake ni dhaifu. Ndugu ´Aliy al-Hijiriy amebainisha udhaifu wake katika uchunguzi ambao umepambanuka. Amekusanya mapokezi yote yanayotumiwa kama dalili na Ahl-ul-Hadiyth. Kadhalika Hasan as-Saqqaaf amebainisha udhaifu wake katika kitabu maalum ambapo amesema ndani yake:

“Ibn-ul-Qayyim amedai kuwa Hadiyth zinazozungumzia kuwa Allaah ataonekana [siku ya Qiyaamah] zimekuja kwa njia nyingi kabisa (Mutawaatir). Mambo sivyo kabisa. Bali ni Hadiyth zilizopokelewa kwa njia moja moja (Ahaad) na zilizotiwa kasoro. Sisi tunaona kuwa zimepokelewa na wana wa israaiyl haijalishi kitu hata kama zitakuwa katika vitabu “Swahiyh”. Zimechomekwa ndani ya Ummah huu na watu kama Ka´b al-Ahbaar, ´Abdullaah bin Sallaam[2] na watu mfano wao.”[3]

[1] Muslim (449).

[2] Tazama https://firqatunnajia.com/abu-az-zurah-kuhusu-anayemtukana-swahahabah-mmoja-tu/

[3] Mas-alah Ru´yah, uk. 05

  • Mhusika: Zakariyyah bin Khaliyfah al-Mahramiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Balsam ash-Shaafi´iy fiy Tanziyh-il-Baariy, uk. 146
  • Imechapishwa: 24/01/2019