Swali: Mimi ni mwanamke nimeolewa na ni mwajiriwa. Nina watoto. Kuna jambo linanikera ambalo nachelewesha swalah ya Fajr. Wakati fulani inakuwa kwa sababu na wakati mwingine inakuwa pasi na sababu. Naomba nasaha na niombee kwa Allaah. Kwani mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.

Jibu: Namuomba Allaah (Ta´ala) amsaidie yeye na sisi juu ya kumkumbuka, kumshukuru na kumtengenezea ´ibaadah Zake. Kuhusu swalah kuwa nzito kwake, nadhani miongoni mwa sababu kuu ni yeye kuchelewa kulala. Mtu anahitajia kulala ili apate kupumzika. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anachukia kulala kabla ya ´Ishaa na mazungumzo baada ya ´Ishaa. Lau atalala mapema na kama ana kazi, kama vile kufanya kidogo marejeo, kujikumbusha n,k. basi akazifanya mwishoni mwa usiku. Aamke na kuswali swalah ya usiku kiasi alichoandikiwa na Allaah kisha arejee yale anayotaka kuyarejea. Kwa sababu kusimamia jambo la kiwajibu la kimasomo ni jambo la lazima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51) http://binothaimeen.net/content/1164
  • Imechapishwa: 01/07/2019