Muweza wa kuumba mbingu ana haki zaidi ya kuwahuisha wafu

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ

“Hakika Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake katika siku sita na wala hatukuguswa na uchovu wowote.” (50:38)

Haya ni maelezo Yake (Ta´ala) juu ya uwezo Wake mkubwa na utashi Wake wenye kutendeka ambao kwavyo ndivo ameumba kiumbe kilicho kikubwa zaidi:

السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ

“… mbingu na ardhi na vilivyo kati yake katika siku sita… “

Siku yake ya kwanza ni jumapili na siku yake ya mwisho ni siku ya ijumaa. Alifanya hivo bila ya kuchoka wala kutaabika. Yule ambaye ameviumba – pamoja na ukubwa na utukufu wake – ni muweza na ana haki zaidi ya kuweza kuwahuisha wafu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym-ur-Rahmaan, uk. 520
  • Imechapishwa: 04/04/2020