318- Ni katika Sunnah kutambua kuwa Mut´ah ni haramu mpaka siku ya Qiyaamah.

319- ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nikipata khabari kwamba kuna mtu ameoa kwa mujibu wa Mut´ah na amejua juu ya uharamu wake, basi nitampiga mawe akiwa tayari ameshaingia kuingia ndani ya ndoa au bakora akiwa ni bikira.”

320-´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) aliletwa bwana mmoja aliyefanya Mut´ah ambapo akasema:

“Lau ningekuwa nimesogea mbele basi ningempiga mawe.”

  • Mhusika: Imaam ´Ubaydullaah bin Battah al-´Ukbariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh wal-Ibaanah, uk. 69
  • Imechapishwa: 09/07/2020