Mume na mke wameingiliana mchana wa Ramadhaan


Swali: Mume wangu aliniingilia mchana wa Ramadhaan kutokana na udhaifu wangu mimi na yeye – tunamuomba Allaah atusamehe. Je, inatosha hivi sasa kuchinja kichinjwa na kukigawa au tulishe masikini mia na sitini au haisihi?

Jibu: Ni wajibu kwa mume na kwa mke kila mmoja katika wao kuacha mtumwa huru, wasipoweza basi kila mmoja afunge miezi miwili mfululizo, wasipoweza kila mmoja alishe masikini sitini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/952
  • Imechapishwa: 10/05/2018