Mume kanuia kumtaliki mke lakini anachelewesha kufanya hivyo


Swali: Ipi hukumu ya mwenye kunuia kumtaliki mke wake na akachelewesha kufanya hivyo?

Jibu: Mwanaume akinuia kumtaliki mke wake kisha akaacha hilo na asifanye kitu, Talaka haipiti. Nia haifanyi Talaka kupita. Kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu yanayohadithia nafsi zao maadamu hawajayafanaya au kuyatamka.”

Maadamu hajayatamka na wala kuyafanya – kuandika hilo – isipokuwa kaweka nia tu, nia hii haipitishi chochote na mke atabaki katika asli yake. Talaka haipiti mpaka aandike Talaka au aitamke.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 18/03/2018