Swali 878: Shari´ah inasemaje juu ya mwanamke ambaye mume wake ni mwenye kuacha swalah na anakunywa pombe?

Jibu: Ana haki ya kuomba talaka. Kwa sababu kuacha swalah, japo ni kwa uvivu, ni ukafiri. Haya ndio maoni sahihi. Mlevi anaweza kumuua yeye au akamuua mtoto wake.

Kuhusu mahari ikiwa yeye mwanamke ndiye kaomba talaka na hakimu akaona kuwa aikomboe nafsi yake kwa kiwango kadhaa cha pesa basi amkabidhi. Hakimu akimlazimisha mume kumtaliki basi [mke] atachukua mahari yake yote. Hapo itakuwa ni lazima kwa mume kumhudumia na kumvisha ndani ya muda wa eda.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 3501
  • Imechapishwa: 26/07/2019