Swali: Mume wangu anafungua barua zangu zinazonijia kutoka kwa familia yangu na anazisoma, jambo ambalo lanichukiza. Ananikataza zile barua ambazo zinahusu kutoa pole ilihali mimi ni mwenye kuhitajia hilo. Je, ana haki ya kufanya hivo?

Jibu: Haifai kwa mume wala asiyekuwa mume kufungua yaliyomo ndani ya barua. Huku ni kumfanyia vibaya yule mwenye barua hiyo. Ni jambo lisilo na shaka kwamba barua iliofungwa ni siri. Haifai kwa yeyote kuisoma.

Mimi namnasihi mume huyu na kumukhofisha juu ya Allaah (´Azza wa Jall). Je, wewe unaridhia yeyote afungue yaliyomo ndani ya barua yako? Naamini kuwa yeye haridhii. Ikiwa yeye hayuko radhi yeyote kufungua yaliyomo ndani ya barua yake, ni kwa nini anajihalalishia kufungua yaliyomo ndani ya barua ya mke wake? Namtahadharisha juu ya hayo. Namwambia: yaliyopita kwa mke wako hayo yameshapita na tubu kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/807
  • Imechapishwa: 05/02/2018