Muhaddithuun wana uelewa wa juujuu

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa Muhaddithuun hawana uelewa; na kwamba fahamu zao ni za juujuu na kwamba ufahamu wa Fuqahaa´ ndio wenye kuingia kwa ndani. Unasemaje juu ya hilo? Haya yanasemwa na baadhi ya wanafunzi.

al-Albaaniy: Wanaosema maneno haya wao wenyewe ni Fuqahaa´?

Muulizaji: Sidhani hivo.

al-Albaaniy: Hapana shaka kwamba wao sio Fuqahaa´. Bali ni wajinga. Hebu wape baadhi ya mambo ya kisasa kisha utaona namna watakavoyafumbua. Hakuna faida kubwa ya kuraddi uchokozi wa watu hawa. Ni kuwarejesha katika msingi; wakiitikia ni sawa na la sivyo tunawaambia:

قُل لَّا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ

“Sema: “Hamtoulizwa juu ya ule uhalifu tulioufanya na wala hatutoulizwa kwa yale mnayoyatenda.”[1]

[1] 34:25

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (7) Dakika: 00:30
  • Imechapishwa: 22/06/2021