Muda ambao mara nyingi mke anaweza kumsubiria mume wake aliye mbali

Swali 06: Ni muda kiasi gani ambayo ni lazima kwa mke kumsubiria mume wake katika jimaa?

Jibu: Muda ambao mara nyingi mwanamke anaweza kumsubiria mume wake ni miezi mine. Huo ndio muda ambao Shari´ah imekadiria juu ya mume ambaye ameapa kuwa hatomwingilia mke wake. Muda huu ndio bora zaidi unaoweza kukadiriwa kizama ambapo mwanamke anamsubiria mume wake kwa nisba ya jimaa. Amesema (Ta´ala):

  لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao wangojee miezi minne. Wakirejea basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 02:226

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (19/339)
  • Imechapishwa: 30/06/2019