Mtubiaji amepata chakula wakati wa funga yake

185- Baba yangu amesema:

“Amenieleza kwamba ikiwa mtu ambaye analazimika kutoa kafara kwa ajili ya kuvunja kiapo chake na akakosa chakula cha kuwapa masikini na hivyo akawa amefunga siku siku moja au mbili; basi anatakiwa kuendelea na funga yake hata kama atapata chakula wakati amefunga. Vivyo hivyo inahusiana na mtu ambaye amemfananisha mke wake na mgongo wa mama yake na muuaji. az-Zuhriy amesema:

“Kwa yule ambaye ameianza kafara yake kwa kufunga na baadaye akapata chakula Sunnah ni yeye kuendelea kufunga.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/140-141)
  • Imechapishwa: 26/03/2021