Mtu atapimwa na matendo yake siku ya Qiyaamah


Swali: Je, mtu mwenye matendo atapimwa na matendo yake?

Jibu: Ndio, ndio dhahiri. Atapimwa mtu mwenye matendo na matendo. Amesema (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا

“Hao ni wale waliozikanusha alama za Mola wao na [pia wakakanusha] kukutana Naye basi ‘amali zao zimeporomoka; hivyo Hatutowapimia Siku ya Qiyaamah uzito wowote.” (18:105)

Kafiri hana ya kupimiwa kwa kuwa hana matendo yoyote. Kuhusu muumini atapimwa yeye na matendo yake.

Siku moja Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) alipanda mti na watu wakacheka juu ya wembamba wa muundi wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Miundi yake siku ya Qiyaamah itakuwa na uzito kuzidi jibali la Uhud.”

Ni dalili inayoonyesha kuwa muumini na yeye atapimwa siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_11.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2018