Mtu anataka kuswali peke yake swalah ya kuomba mvua

Swali: Inajuzu kwa mtu akaswali peke yake swalah ya kuomba kuteremshiwa mvua au mwalimu pamoja na wanafunzi wake masomoni?

Jibu: Kujengea maoni ya Fuqahaa´ (Rahimahumu Allaah) inafaa akaswali peke yake, mtu pamoja na familia yake nyumbani au masomoni. Lakini Sunnah kamilifu ni mtu akakusanyika pamoja na waislamu wengine sehemu moja na kwa kuwepo imamu mmoja na wakamuomba Allaah. Kwa sababu kila ambavo watu watakusanyika kwa wingi ndivo uwezekano wa kujibiwa unakuwa mkubwa zaidi.

Kwa ajili hiyo tunawanasihi ndugu zetu kuhudhuria kwa wingi mahali pa kuswalia swalah ya ´iyd. Fuqahaa´ wamesema mtu atoke kwenda mahali pa kuswalia swalah ya ´iyd akiwa pamoja naye wazee, watoto ambao wameshakuwa na uwezo wa kupambanua mambo na watu wema. Kwa sababu hilo liko karibu zaidi na kuweza kujibiwa. Hili ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (60) http://binothaimeen.net/content/1369
  • Imechapishwa: 28/11/2019