Mtoto wa miaka saba anamsifu mama yake mdogo kwa baba yake


Swali: Mtoto wa miaka saba anamweleza baba yake jinsi mama yake mdogo anavofanana.

Ibn ´Uthaymiyn: Unakusudia kwamba anamsifu mwanamke huyu kwa wanamme wa kando naye?

Muulizaji: Ndio. Ni ipi hukumu ya mtoto huyu kuwa kati ya wanawake?

Jibu: Huyu hatakiwi kuwepo kati ya wanawake. Ni lazima kwake kujifunika mbele yake. Amesema (Ta´ala):

أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ

“… au watoto ambao [bado] hawaelewi [kitu kuhusu] yanayohusu uke.”[1]

Hili liko wazi. Muda wa kuwa anajua sifa na anaweza kupambanua ni wepi wanawake warembo na wasiokuwa warembo ni lazima kujiepushe naye.

Swali: Hata kama ni mama yake mdogo?

Jibu: Anapaswa kukatazwa jambo hili. Midhali ni mama yake mdogo hawezi kujisitiri mbele yake, lakini anapaswa kukatazwa kufanya hivo. Ni wajibu wamfunze kwamba kitendo hicho ni kibaya na kumtishia vile wanavoweza.

[1] 24:31

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (11 B) Dakika: 35.40
  • Imechapishwa: 03/07/2021