Mtoto ameacha kufunga ilihali kishabaleghe

Swali: Kuna mtu amebaleghe lakini hata hivyo akaacha kufunga Ramadhaan kwa kufikiri kuwa kufunga sio wajibu isipokuwa kwa ambaye kishafikisha miaka kumi na tano. Ni lipi linalomlazimu?

Jibu: Ni wajibu kwake kulipa. Isipokuwa tu ikiwa kama yuko sehemu waliyoko sehemu hiyo ni wajinga na mwanachuoni yeyote ambaye angeliweza kulitazama jambo lake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/91)
  • Imechapishwa: 31/05/2017