Mtalikiwa baada ya ndoa hurudi kwa hesabu ya talaka alizotalikiwa


Swali: Kuna mwanamume alimtaliki mke wake talaka rejea na hakumrudi mpaka eda yake ikawa imeisha. Baada ya hapo akamuoa tena kwa ndoa mpya. Je, ile talaka ya kwanza inahesabika kwake?

Jibu: Akimtaliki na akatoka katika eda, basi anazingatiwa ni mposaji katika waposaji kama wengine. Katika hali hii anatakiwa kumuoa kwa kufunga naye ndoa mpya, awepo walii na mahari. Akimuoa basi kumebaki kwake talaka mbili. Ile talaka ya kwanza inahesabika kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 07/03/2018