Swali: Mashaykh wengi wa nchi yetu ni Suufiyyah. Wanahalalisha kuyatembelea misikiti yenye makaburi na mawalii kwa madai yao na kuswali kwao. Wakati wanapoulizwa kama inafaa kumuomba msaada al-Husayn na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanasema ndio na kwamba ni katika njia zilizowekwa katika Shari´ah. Ni ipi kuraddi hilo na ni ipi hukumu ya maneno haya?

Jibu: Maneno haya ni batili. Hii sio njia iliowekwa katika Shari´ah. Bali haya ni katika batili iliokatazwa. Kama tulivosema ni lazima kwenu kuwabainishia kwa hekima na maneno mazuri  na kujadiliana nao kwa njia iliokuwa bora zaidi. Msinyamaze.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (93) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighstah%20-20-1-1440_0.mp3
  • Imechapishwa: 13/04/2019