Msingi wa Raafidhwah uko katika uzandiki na ukafiri

Ama Raafidhwah, msingi wa Bid´ah yao iko katika uzandiki na ukafiri. Kukusudia uongo ni jambo limekithiri kwao. Wao wenyewe wanalikubali hilo pale wanaposema:

“Dini yetu sisi ni Taqiyyah.”

Maana yake ni mtu kusema kwa mdomo wake kile asichokiamini moyoni mwake. Hiki si kingine isipokuwa ni uongo na unafiki. Pamoja na haya wanasema kwamba wao ndio waumini na si waislamu wengine wote. Aidha wanawatuhumu wale wa mwanzo waliotangulia kuritadi na unafiki. Wao ni kama ule msemo unaosema:

“Imeingiia sumu yake na ikayayuka.”

Hata hivyo hakuna yeyote anayeonyesha Uislamu ambaye yuko karibu zaidi na unafiki na kuritadi kama wao. Hakuna kundi lolote lililo na wenye kuritadi na wanafiki wengi kama wao.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/68-69)
  • Imechapishwa: 29/01/2019