Msimamo wa waislamu kwa mtawala anayehukumu kwa kanuni


Swali: Sisi tunaishi katika nchi ambayo inahukumu kwa kanuni za kikafiri. Vipi unatakiwa uwe msimamo wetu kwa watawala hawa? Je, tuwahukumu ukafiri au tuwafanyie uasi?

Jibu: Msiwafanyie uasi kwa vile hatujui udhuru wao. Huenda wakawa na udhuru msiyoujua. Allaah ndiye anajua zaidi. Nchi hiyo ikiwawia dhiki kwenu tokeni na kuhama kwenda nchi nyingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 01/05/2018