Msimamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya maneno ya Allaah (´Azza wa Jall)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika sifa Zake za kimatendo ni kwamba anazungumza. Kama ambavyo anaumba, anaruzuku, anahuisha na kufisha, anaendesha mambo, anapenda na kutaka (Subhaanahu wa Ta´ala) vilevile anazungumza maneno yanayolingana na utukufu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) kama zilivyo sifa Zake zingine. Anazungumza pindi anapotaka, anachokitaka na namna anayotaka.

Maneno Yake anazungumza anapotaka. Alizungumza kwa Qur-aan wakati wa kuteremka Kwake, anamzungumzisha Jibriyl, alimzungumzisha Muusa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku alipandishwa mbingu. Kabla ya hapo alimzungumzisha Aadam (´alayhis-Salaam) na atazungumza siku ya Qiyaamah akiwafanyia watu hesabu. Atawazungumzisha waumini Peponi nao watamzungumzisha. Kwa hivyo anazumgumza kwa maneno aina yake ni ya tagu hapo kale na yanatokea kwa wakati mbalimbali kutegemea na tukio.

Vitabu vyote walivyoteremshiwa Mitume vyote ni maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Miongoni mwayo ni Qur-aan tukufu ambayo ndio kubwa yavyo na Allaah amejaalia kuwa ndio yenye kuvihukumu. Kwa hivyo Qur-aan ni maneno Yake (Jalla wa ´Alaa) ya kihakika na sio Majaaz. Qur-aan imeteremka kutoka Kwake na haikuumbwa. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wanayasema haya kwa mdomo mpana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Haa-iyyah, uk. 44