Msimamo sahihi kati ya walinganizi na watawala


Swali: Ni ipi hukumu ya walinganzi wa Tawhiyd kubomoa makaburi [baki ya swali haliko wazi]…

Jibu: Ibn ´Abdil-Wahhaab hakubomoa makuba peke yake na wala hakuwapiga mawe wazinifu peke yake. Alikuwa na watawala baada ya kulingania kwa Allaah na baada ya kumkinaisha mtawala, kama nilivyotaja katika jawabu la kwanza. Hakutaki tamaa Allaah kumwongoza mmoja katika watawala. Ni lazima kwa walinganizi kuwasiliana na watawala na wawalinganie kwa Allaah kwa hekima, maneno mazuri na wawawekee wazi na wala wasikate tamaa. Hawatakiwi kukata tamaa. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yukaribu na mwenye kuitikia. Nyoyo ziko mikononi mwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Lakini sisi sisi kujitenga na kuwatukana watawala mbele ya umati na kugombana nao ni jambo linalosababisha fitina. Ni lazima uwasiliane nao. Ni lazima uwanasihi. Ni lazima uwape mawaidha kwa njia nzuri. Uyafanye yote hayo kwa kutumia hekima na maneno mazuri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema kumwambia Muusa na Haaruun (´alayhimas-Salaam) wakati alipowatuma kwa Fir´awn:

فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Mwambieni maneno laini huenda akawaidhika au akaogopa.” (20:44)

Hawa ni Mitume wawili watukufu wakiwa pamoja na mjeuri huyu ambaye anadai kuwa yeye ndiye mungu. Pamoja na haya yote Allaah anawaambia:

فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Mwambieni maneno laini huenda akawaidhika au akaogopa.”

Hii inafahamisha kwamba wanatakiwa kuambiwa uso kwa uso kati yako wewe na yeye. Sio wewe uko sehemu ya mbali unatukana na kuwaapiza. Hili linasababisha fitina zaidi. Lakini unachotakiwa ni wewe kuwaambia maneno laini. Maneno yasiyokuwa na ususuwavu na ukali matokeo yake ukaja kuwakimbiza. Ni lazima kufuata mfumo wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Vinginevyo Da´wah haitofaulu. Matokeo yake utakuja kuchoka bure pasi na faida.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Masaa´il-il-Jaahiliyyah (01) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/jahlyh_01.mp3
  • Imechapishwa: 18/11/2017