Swali: Nina miaka mingi ambayo sikufunga nilipokuwa mdogo na sikumbuki ni lini nilijiwa na ada ya mwezi. Ni kipi kinachonilazimu hivi sasa?

Jibu: Ni lazima kwa mwanamke kufunga pale anapobaleghe kwa hedhi, kwa kuota au kwa kufikisha miaka kumi na tano. Ni lazima kujitahidi kufanya uchunguzi na kulipa ikiwa uko na deni juu ya miezi ambayo hukufunga. Sambamba na hilo unatakiwa kutoa chakula ya 1,5 kg ya mchele au ngano kwa kila siku moja iliyokupita.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mufti.af.org.sa/ar/content/%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%83-%D8%B5%D9%8A%D8%A7%D9%85-%D9%85%D8%A7-%D9%81%D8%A7%D8%AA%D9%83-%D9%85%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%A5%D8%B7%D8%B9%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 01/05/2020