Swali: Nimesikia kuwa kunyoa kichwa ni katika sifa za Khawaarij na kufanya hivo nje ya Hajj na ´Umrah ni Bid´ah. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Bid´ah ni maneno haya. Haya ndio Bid´ah. Kunyoa kichwa imeruhusiwa na kuziacha nywele kwa sifa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Sunnah. Ama kuhusu kukinyoa imeruhusiwa. Tokea kabla ya Khawaarij watu walikuwa wakinyoa vichwa vyao. Kadhalika baada ya Khawaarij watu waliendelea kunyoa vichwa vyao. Kufanya hivo wakati wa haja hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-6-9.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014