Msafiri anayejua haja yake haitoisha chini ya siku nne


Swali: Anayesafiri kwenda katika mji masafa ya kujuzu kufupisha. Akakaa hapo kwa haja na hajui ni lini haja yake itaisha na wakati itapoisha atarejea. Hata hivyo anajua kuwa atakaa zaidi ya siku nne. Je, anapata rukhusa kama ya msafiri hata kama muda utakuwa mrefu?

Jibu: Huyu anajua kuwa atakaa zaidi ya siku nne kwa kuwa haja yake haitoisha ndani ya siku nne. Huyu anakuwa ni mkazi. Haijuzu kwake kuchukua rukhusa za safari. Kwa kuwa anajua haja yake itakuwa haikuisha ndani ya siku nne.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-04-15.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014