Msafiri anafupisha kwa hali zote na anakusanya wakati wa haja


Swali: Tunaomba utuwekee wazi juu ya yale yaliyopokelewa katika Sunnah kwamba walikuwa wakikusanya swalah pindi wanapokuwa na uzito. Vipi endapo msafiri amesimama safari yake inakuwa imekatika? Ni ipi hukumu ikiwa ule muda ulio kati yake yeye na mji wake unakaribia kuweza kuwahi ule wakati wa swalah ya pili? Katika hali hii afupishe na kukusanya?

Jibu: Sahihi ni kwamba akusanye. Hilo ni kwa sababu kufupisha ni Sunnah kwa msafiri. Ni mamoja awe na urahisi au uzito. Kuhusu kukusanya kati ya swalah mbili ni Sunnah kwa msafiri kufanya hivo pale anapokuwa na uzito au kwa msemo mwingine pale anapokuwa yuko safarini anatembea. Ama akiwa ametua sehemu au katika mji asikusanye. Endapo atakusanya hakuna neno. Kufupisha ni Sunnah kwa hali yoyote. Kuhusu kukusanya ni Sunnah pale msafiri anapokuwa na ugumu. Vinginevyo bora asikusanye. Iwapo atafanya hivo hakuna neno.

Ama ikiwa msafiri amefika katika mji na akajua kuwa atafika katika mji wake kabla ya kuingia wakati wa swalah ya pili, tunasema kuwa inafaa kwake kukusanya. Lakini bora katika hali hii asikusanye. Kwa sababu hakuna haja ya ujumuishaji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/802
  • Imechapishwa: 05/02/2018