Mnyonyeshaji anadhurika kwa kufunga


Swali: Swawm ikiwa ngumu kwa mwanamke myonyeshaji. Inajuzu kwake kuacha kufunga?

Jibu: Ndio, inafaa kwake kuacha kufunga ikiwa swawm ni ngumu kwake au akichelea kupungua kwa maziwa ya kifuani juu ya mtoto wake. Katika hali kama hii inafaa kwake akaacha kufunga na akalipa idadi ya yale masiku yaliyompita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/158)
  • Imechapishwa: 20/05/2019