Mke wangu haswali na wala havai Hijaab, nifanye nini?


Swali: Mke wangu mimi haswali. Na nimeshamwamrisha Swalah zaidi ya mara moja lakini hapokei (nasaha). Hali kadhalika havai Hijaab, na nywele zake zinaonekana na watu wote. Naomba unipe faida nimfanye nini?

Jibu: Mwanamke huyu, kakusanyikiwa na shari mbili kubwa. Na moja wapo ni kubwa zaidi kuliko nyingine.

1) Shari ya kwanza ni kutoswali kwake kwake na hii ni kufuru kubwa kutokana na kauli ya sahihi.

2) Shari yake ya pili, ni kutojisiri kwake kwa Hijaab. Inatakikana kwako na hili ni jambo la wajibu kutengana nae, kwa kuwa haijuzu kwa Muislamu (wa kiume) kubaki na mwanamke kafiri. Anasema (Ta´ala):

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao.” (60:10)

Ni wajibu kwako kutengana nae maadamu hapokei nasaha. Ni wajibu kuachana nae. Na ninakubashiria kuwa utapata aliye bora kuliko yeye. Na (huyo mwanamke) tunamuombea kwa Allaah uongofu. Muhimu ni kuwa, huyu mwanamke ana shari mbili ambazo ni kubwa, na moja wapo ndio kubwa zaidi kuliko nyingine. Nayo ni kuacha Swalah, hii ni kubwa kwa kuwa hii ni kufuru kubwa. Na kule kutojisitiri kwake si nywele zake wala uso wake, hii pia ni dhambi na shari kubwa. Ni wajibu kwako kutengana nae, kutahadhari nae na kumpa Talaka. Tunamuomba Allaah sote Atupe afya. Na yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora kuliko hicho (alichokiacha). Allaah Atakupa aliye mbora na mwema kuliko yeye In Shaa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 19/03/2018