Mke na watoto kula katika pato la baba ambalo ni haramu

Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mtu anakula haramu na yuko na watoto na watu anaowapa?

Jibu: Hali zao zinatofautiana. Yule mwenye kutenzwa nguvu tunatarajia hatopata dhambi. Mfano wa hawa ni wale wavulana, watoto wengine wadogo na mfano wao. Wanawangalia yeye. Yeye ndiye anayepata dhambi.

Kuhusu mke ambaye anajua hili ni lazima kwake kuomba talaka na atengane naye. Huu ni udhuru wa Kishari´ah. Ikiwa pato lake ni chafu, basi ni juu yake kuomba talaka na badala yake aende katika nyumba ya familia yake na amtaka abadilishe pato. Vinginevyo amuomba talaka ili asibaki naye wanakula haramu pamoja naye.

Lakini akiwa na pato la halali lakini hata hivyo lililochanganyika na baadhi ya mali isiyokuwa nzuri, hili ni sahali kidogo na jambo hili ni pana. Ama akiwa anatambulika kuwa ana pato la haramu au ikawa chumo lake lote ni haramu, basi mke huyu ana udhuru na watoto wake wana udhuru wa kutokula nyumbani kwake. Kunamaanishwa wale watoto wake wakubwa watuwazima ambao wameshapevuka. Kuhusu wale watoto wake wadogo waliotenzeka nguvu na wale mafakiri wasiokuwa na njia nyingine yoyote, natarajia kuwa Allaah atawasamehe endapo watakula kutoka katika mali yake wakati wa dharurah mpaka pale Allaah atapowajaalia njia ya kutokea.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.binbaz.org.sa/noor/3109
  • Imechapishwa: 08/01/2017