Mke hataki kukoga janaba na anajua ni wajibu


Swali: Ipi hukumu ya mwanamke ambaye hakogi janaba naye anajua kuwa kukoga ni wajibu?

Jibu: Atazingatiwa kuwa ni mfanya madhambi na anafanya Haramu. Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا

“Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni.” (05:06)

Wajibu kwa Muislamu ni yeye kukimbilia kujitwahirisha kunapokuja wakati wa Swalah. Ama lau maingiliano yatakuwa mwanzoni mwa usiku, mume wake anaweza kutangulia kukoga kisha akafuata mke au wakakoga wote wawili. Wanaweza vile vile kuchelewesha mpaka kabla ya Fajr. Hakuna ubaya kwa hili. Katika hali hii itabidi watawadhe. Hakuna ubaya kufanya hivi. Na kunapokuja wakati wa Swalah, ni wajibu kwake mwanamke ajitwahirishe na aswali. Na kunapokuja wakati wa Swalah asijitwahirishe wala kuswali, huku kutokuswali kwake anazingatiwa kuwa ni kafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2431
  • Imechapishwa: 27/02/2018