Mke asitoke nyumbani pasina idhini yako


Swali: Nilimkataza mke wangu kutoka kwenda harusini, lakini hakunitii. Akaenda na akatumia hoja ya kwamba mama yake alitaka amfuate na kwamba angelikuwa amemuasi mama yake ikiwa atanitii mimi.

Jibu: Hapana, sio muasi kabisa kwa mama yake. Ikiwa kuna maasi kwenye harusi itakuwa ni dhambi kwenda. Hatakiwi kumtii mama yake juu ya hilo. Badala yake anatakiwa kumnasihi mama yake na si kwenda huko. Anafanya sawa ikiwa hatoenda huko. Kwa kuwa anataka kuepuka maasi. Hini ni jambo la kwanza.

Jambo lingine ni kwamba hatakiwi kutoka nyumbani kwako pasina idhini yako. Una majukumu juu yake. Haijuzu kwake kutoka nyumbani kwa mume pasina idhini yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg--14340329.mp3
  • Imechapishwa: 22/09/2020