Misri, Siyria, ´Iraaq na Libya – hapo kabla na hivi sasa


Hebu wacha tutazame Misri. Je, Misri imekuwa bora kabla au baada ya mapinduzi? Waalimu wa kimisri walitufunza katika kipindi ambapo Misri ilikuwa nchi ya kifalme na wakatufunza baada ya nchi kuwa ya ufalme. Kipindi hicho paundi moja ya kimisri ilikuwa ni zaidi ya SAR kumi. Hivi sasa mnajua thamani yake.

Wakati muungano kati ya Misri na Syria ulipovunjika yakazuka mapinduzi Syria. Kwa kuongezea ni muungano ambao haukuwa wenye kufanikiwa tangu mwanzo. Ilikuwa ni kana kwamba walitumbukia ndani ya dinbwi lisilokuwa na mwisho.

´Iraaq mtawala alikuwa anatokamana na familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kutoka katika ash-Shariyf Husayn, babu yake na Husayn aliyefariki Jordan. Kisha yakatokea mapinduzi. Kabla ya hapo Ahl-us-Sunnah ´Iraaq walikuwa ndio wengi zaidi. Baada ya ufalme hali ´Iraaq ikawa mbaya zaidi siku baada ya siku. Kuhusu hali ya ´Iraaq hivi sasa, hakuna haja ya kuizungumzia.

Nchi zote ambazo kumetokea mapinduzi na shari zimepewa mtihani.

Wakati wa mfalme Idriys as-Sanuusiy Libya ilikuwa nchi tulivu. Baadaye al-Qadhaafiy akafanya mapinduzi na nchi ikawa mbaya zaidi. Kwa ajili hiyo ndio maana muislamu anatakiwa kufikiria matokeo ambayo ni natija ya kuiacha Sunnah juu ya yale yanayohusiana na kuheshima na kutukuza kiapo.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa Tarehe: 1436-02-05/2014-11-27
  • Imechapishwa: 15/06/2021