Miongoni mwa watenda maasi wenye adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watengeneza picha

Swali: Ni vipi tutaoanisha kati ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Hakika watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale wanaoigiza maumbile ya Allaah.”

na kwamba washirikina ndio watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah?

Jibu: Kumetajwa katika uoanishaji yafuatayo:

Ya kwanza: Hadiyth inamaanisha kuwa kuna miongoni mwa watu kwa dalili ya kwamba imesema:

“Hakika watu wataokuwa na adhabu kali… “

Kwa hivyo inafasiriwa kama ilivyothibiti ya kwamba kuna miongoni mwa watu.

Ya pili: Ukali wa adhabu haimaanishi ya kwamba wengine hawatoshikiana nao. Bali kuna ambao watashirikiana nao. Amesema (Ta´ala):

وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ

“Siku itakayosimama Saa [itasemwa] “Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali.” (40:46)

Kwa hiyo wote wanakuwa ni wenye kushirikiana katika adhabu. Lakini hili linaweza kupingwa kwa kusema ya kwamba mtengeneza picha ametenda dhambi kubwa na ni vipi ataweza kulinganishwa na ambaye ni kafiri na mwenye kiburi.

Ya tatu: Ukali wa adhabu ni wa kinisba. Kwa msemo mwingine ni kwamba watengeneza picha ni wenye adhabu kali ukilinganisha na watenda madhambi wengine ambao madhambi yao hayakufikia ukafiri na sio kwa nisba ya watu wote. Hii ndio tafsiri ilio karibu zaidi na usawa na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/281-282)
  • Imechapishwa: 03/07/2017