Miaka ya kumpeleka mtoto msikitini

Swali: Ni umri upi muafaka wa kumpeleka mtoto msikitini ili azowee swalah?

Jibu: Pale anapokuwa ni mwenye uwezo wa kupambanua. Anapokuwa ni mwenye uwezo wa kupambanua na chinichini inakuwa miaka saba:

“Waamrisheni watoto wenu swalah wanapokuwa na miaka saba na wapigeni kwayo wanapokuwa na miaka kumi.”

Ama mtoto akiwa chini ya miaka saba na mzazi akampeleka kwa ajili ya kumlinda, hakuna neno ilimradi mtoto asiwasumbue wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017