Mguu mmoja ndani katika Salafiyyah, mwingine nje kwenye Hizbiyyah


Swali: Mtu akiwa ni mwenye kukimbilia Salafiyyah. Lakini hata hivyo akawa bado yuko na athari zilizotangulia. Je, atupiwe macho mpaka pale atapoisalimisha nafsi yake na Salafiyyah?

Jibu: Ndio, atupiwe macho. Abainishiwe yale anayotumbukia ndani yake. Anaendelea katika udhaifu huu na kurudi nyuma huku? Anatakiwa kubainishiwa na kuelekezwa katika vitabu ambavyo anaweza kuvisoma ili aisalimishe nafsi yake. Kwa sababu huku kuyumbayumba kunadhuru na khaswa yule ambaye amekulia katika nchi hii. Mfumo uko wazi. Hana udhuru juu ya kuchanganyikiwa na kudhoofika. Lakini hata hivyo sisi tunakomaa nae na tunamsubiria mpaka pale atapojisalimisha.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda: Sabiyl-in-Naswr wat-Tamkiyn http://rabee.net/ar/questions.php?cat=27&id=206
  • Imechapishwa: 11/02/2018