Mfumo wa Salaf uliopo leo umezuliwa?


Swali: Kuna wenye kusema kuwa mfumo wa Salaf uliopo hii leo ni mfumo uliozushwa ambao umezushwa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwajeruhi watu na kuwatoa katika Sunnah. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Huku ni kujigonga. Vipi itakuwa ni mfumo wa Salaf kisha uwe umezushwa? Salaf ni kitu kimetangulia; ni mfumo wa Maswahabah na wale wenye kuwafuata kwa wema. Huu ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Yaliyozushwa ni yale yaliyokuja baada yake. Ama kuhusiana na mfumo wa Salaf ni wenye kuendelea. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Wakasema: “Ni kina nani hao?” Akasema: “Ni wale wataokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Yule ambaye anafuata yale aliyokuwemo Mtume na Maswahabah zake ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Kilichozushwa ni maneno yake haya ya batili. Maneno haya ndio yamezushwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 11/04/2018