Mfanyakazi mwanamke kusafiri nchi za nje bila Mahram

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia mfanyakazi mwanamke katika nchi ya kiislamu pasi na Mahram kutokana na haja ya kidharurah?

Jibu: Ni lazima kwa wanawake wote wasisafiri isipokuwa kwa kuwa pamoja na Mahram. Ni mamoja mfanyakazi mwanamke au mwengine. Kila mwanamke ni lazima awe na Mahram yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke asisafiri isipokuwa pamoja na Mahram.”

Hilo ndilo la wajibu kwa wote. Ni lazima kwa familia yake kumtafutia Mahram.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21523/حكم-استقدام-خادمة-مسلمة-بدون-محرم-لحاجة
  • Imechapishwa: 21/08/2022