Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahmad bin ´Abdillaah ni kwamba amesema:

“Yule mwenye kuamini kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) atarejea ulimwenguni ni kafiri, na yule mwenye kusema kuwa Qur-aan imeumbwa ni kafiri.”

Imesemekana kwamba alikimbia magharibi ya Afrika wakati kulipotokea fitina ya kuumbwa kwa Qur-aan. Akafanya magharibi ya Afrika ndio makazi yake na akapata kizazi huko.

Yahyaa bin Ma´iyn aliulizwa kuhusu Ahmad bin ´Abdillaah bin Swaalih ambapo akajibu:

“Ni mwaminifu, mtoto wa mwaminifu.”

Baadhi yao wamesema kuwa Ahmad bin ´Abdillaah aliishi Tripoli ili aweze kupata faragha na kufanya ´ibaadah. Kaburi lake liko pwani na kaburi la mwanae liko pambizoni mwake. Ahmd al-´Ijliy amesema:

“Nilisafiri kwenda kwa Abu Daawuud at-Twayaalisiy. Akafariki siku moja kabla ya mimi kufika Baswrah.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/506-507)
  • Imechapishwa: 25/11/2020