Maulidi ni Bid´ah yenye kukaripiwa


Allaah na Malaika Wake wamemswalia na akawaamrisha wamswalie na kumtolea salamu. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Hivyo enyi walioamini mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”[1]

Lakini hakutengwi wakati wala namna maalum ya kumsifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa kwa dalili sahihi kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Yale yanayofanywa na watu wa maulidi kutenga siku maalum ambayo wanadai kuwa ndio siku aliyozaliwa ni Bid´ah yenye kukemewa.

[1] 33:56

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 156
  • Imechapishwa: 17/11/2019