Matabano online


Swali: Ni jambo linalokubalika Kishari´ah na lenye kuathiri kumfanyia matabano aliyerogwa au mgonjwa kwa njia ya simu au tv?

Jibu: Halikubaliki Kishari´ah na wala haliathiri kitu. Huu ni mchezo. Ni lazima matabano yawe kwa njia ya moja kwa moja kwa yule aliyesibiwa. Anatakiwa kumsomea na kumtemea cheche za mate moja kwa moja. Kuhusu matabano mtu yuko upande mwingine wa ardhi kwa njia ya simu au njia zengine za mawasiliano si jengine isipokuwa ni hadaa tu na uongo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (60) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16548
  • Imechapishwa: 10/09/2017