Masuala ya talaka tatu yanahitajia ufafanuzi


Swali: Ipi hukumu ya kuapa kwa Talaka mara tatu? Je, Talaka inapita ikiwa kuapa kwake hakumkusudia mke na khaswa isitoshe baadhi ya watu wanafanya hivyo na hawakusudii Talaka? Na ni ipi kafara ikiwa Talaka inapita? Na je, imepita moja au mbili?

Jibu: Talaka tatu kunahitajika ufafanuzi na hatuwezi kuchukulia kwa juu juu. Ni lazima aulizwe mtu huyo aliyetamka hivyo na yajulikane makusudio yake, na matamshi aliyosema na kama hapo alitangulia kutoa Talaka au hapana. Huyu anatakiwa ahudhurie ima mahakamani kwa Qaadhiy au Daar al-Iftaah. Ama kutoa Fatwa ya jumla hapa katika Darsa Msikitini, hili sio sahihi. Kwa kuwa baadhi ya watu wanaweza kufahamu makosa na akaenda kuwaeleza watu alivyofahamu nao wakafahamu makosa. Haya ni lazima apelekewe Muftiy au Qaadhiy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10053
  • Imechapishwa: 03/03/2018