Wale wenye kupinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah pale walipojibiwa kwa majibu haya[1] wakasema kupinga kwetu kuwa Allaah ataonekana Aakhirah kumetokamana na akili yetu inatwambia kuwa ni muhali kumuona Allaah (Ta´ala). Ni jambo lisiloingia akilini. Wao wanaonelea – kama itakavyokuja katika dalili zao huko mbele – ya kwamba Allaah hana kiwiliwili, hayuko ndani ya ulimwengu wala nje yake, kitu chenye sifa kama hiyo hakiwezi kuonekana. Ni jambo lisiloingia akilini ikawezekana.

Ahl-us-Sunnah wakawajibu kwamba kusema kwenu kuwa akili inahukumu kuwa kuonekana kwa Allaah ni jambo ambalo ni muhali, haya ni madai yenu nyinyi. Jambo hili wameenda kinyume na nyinyi watu wengi ambao wana akili. Jambo hili likipelekwa kwenye akili iliosalimika na timamu na ya kimaumbile, basi haiwezi ikahukumu kuwa kuonekana kwa Allaah ni jambo ambalo ni muhali.

[1] Tazama 1287

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/229)
  • Imechapishwa: 30/05/2020