Murji-ah wanasema kuwa hakufuru yoyote isipokuwa tu yule mwenye kukanusha kwa moyo wake. Tumesema kuwa hili ni kosa. Kufuru iko sampuli mbali mbali; inakuwa kwa moyo na kuamini, kwa maneno, kwa matendo, kwa kutilia shaka na kwa kuacha. Lakini hata hivyo ni lazima yatimie masharti na kusipowe vizuizi kwa yule mwenye kufanya kufuru ili aweze kuhukumiwa ukafiri. Masharti yenyewe ni haya yafuatayo:

Ya kwanza: Mtu awe na ujuzi wa anachokisema. Endapo mtu ni mjinga na mtu kama yeye anaweza kuwa hajui kweli, basi hakufuru mpaka asimamishiwe hoja.

Ni lazima vilevile awe ni mwenye khiyari na moyo wake umetua juu ya imani. Ikiwa ametenzwa nguvu hakufuru. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ

“Atakayemkufuru Allaah baada ya imani yake… ” (16:106)

Ya pili: Ni lazima akusudie. Ikiwa hakukusudia kitendo, hawi kafiri. Kwa mfano akikusudia kusujudia sanamu au kutamka neno la kufuru, anakuru. Haishurutishwi aamini ndani ya moyo wake. Lakini hata hivyo ni lazima kuzingatia makusudio. Akifanya au kutamka kitendo pasina kukusudia, hakufuru. Kwa mfano mwendawazimu hana makusudio. Hivyo atapotamka neno la kufuru, hakufuru. Vilevile mlevi, mtoto mdogo na mtu ambaye amepoteza akili, hawa hawana makusudio. Kadhalika mtu ambaye ulimi umemteleza na hakukusudia hivo, kama mfano wa yule mtu aliyesema:

“Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye mja Wangu na mimi ndiye mola Wako.” Muslim (2747).

Ni lazima kutimie masharti haya na kusiwepo vizuizi ili kumhukumu mtu ukafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/528-529)
  • Imechapishwa: 18/05/2020