Swali: Manii yanayotoka baada ya kuoga [janaba] yanawajibisha kuoga tena au yanatengua wudhuu´?

Jibu: Ndio, yanatengua wudhuu´. Kinachotoka kupitia njia mbili kinatengua wudhuu´, sawa ikiwa ni manii au sio manii.

Swali: Kinawajibisha kuoga tena?

Jibu: Hapana. Isipokuwa akihisi ladha na yakatoka na nguvu kwa kuruka. Akihisi ladha na yakatoka na nguvu, hii itakuwa ni janaba na atatakiwa kuoga. Ama kutoka tu bila ya ladha, hili linawajibisha wudhuu´ tu. Aoshe tupu yake na atawadhe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888
  • Imechapishwa: 16/11/2014