Manhaj-ul-Muwaazanah imezushwa na wajinga


Swali: Ni yepi maoni yako juu ya Manhaj-ul-Muwaazanah?

Jibu: Sitambui Manhaj-ul-Muwaazanah. Hiki ni kitu kilichozuliwa na baadhi ya wajinga. Sitambui Manhaj-ul-Muwaazanah. Usawa unapatikana kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Yeye ndiye anayepima mema na maovu na anawalipa wenye nayo kwayo. Kuhusu sisi hatujui. Lakini hata hivyo tunamraddi mwenye kukosea. Mwenye kukosea tunamraddi. Haijalishi kitu hata kama atakuwa na mema. Mema yake yanatambuliwa na Allaah. Sisi tunaraddi kosa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 09/12/2017