Swali: Kusema kwamba msichana bikira anapoombwa idhini ya kuolewa basi jibu lake ni kunyamaza ni maneno ya udanganyifu.

Jibu: Haya ni maneno ya kipumbavu. Anachotaka kusema ni kwamba mwanamke bikira anapoulizwa kuhusu kuolewa jibu lake sio kukaa kimya na anasema kwamba huu ni udanganyifu. Haya ni maneno khatari sana kusema kwamba hukumu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni udanganyifu. Mimi sijui vipi mtu anaweza kueneza mambo kama haya katika gazeti na ni vipi kalamu ya mwandishi huyu anaweza kuthubutu kuandika mambo kama haya. Isipokuwa kama atakuwa mjinga hatujui. Anaweza kuwa mjinga asiyejua. Namuomba Allaah amwongoze yeye na sisi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1248
  • Imechapishwa: 25/09/2019