Swali: Nimesoma Hadiyth yenye kusema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayeniswalia kwa siku mara elfumoja, basi hatokufa mpaka abashiriwe Pepo.” Ameipokea Abush-Shaykh kutoka kwa Anas (Radhiya Allaah ´anh)

Je, Hadiyth hii ni Swahiyh, nzuri au dhaifu? Inafaa kuitumia kama hoja? Ikiwa ni Hadiyth Swahiyh ni yepi malengo ya kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hadiyth hii haijasihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila Hadiyth ambayo ndani yake kuna kumuwekea kiwango cha kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni dhaifu. Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo limewekwa kwa njia ya kuachwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kukithirisha kumswalia sana na khaswa siku ya Ijumaa. Ameeleza kuwa swalah zetu anafikishiwa (´alayhi-Swalaatu was-Salaam).

Hivyo, kithirisha kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyakati zote na bila ya kuweka idadi maalum. Atayemswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  mara moja, basi Allaah atamswalia kwa swalah hiyo mara kumi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (26)
  • Imechapishwa: 23/01/2019